Proverbs 5:9-14


9 usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine
na miaka yako kwa aliye mkatili,

10 awageni wasije wakasherehekea utajiri wako
na jitihada yako ikatajirisha
nyumba ya mwanaume mwingine.

11 Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,
wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

12 Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!
Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

13 Sikuwatii walimu wangu
wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

14 bNimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa
katikati ya kusanyiko lote.”

Copyright information for SwhKC